10 Wafariki Ghorofa Likiporomoka

WATU zaidi ya kumi wanahofiwa kupoteza maisha, huku wengine zaidi ya 25 wakiwa wamefukiwa na kifusi, kufuatia kuporomoka kwa jengo la ghorofa tatu katika eneo la Bhiwandi, Mumbai nchini India.

Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo, Septemba 21, 2020, na mpaka sasa, vikosi vya zimamoto na uokoaji vinaendelea na juhudi za kunasua miili  na majeruhi.

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, ametoa salamu za pole kupitia ukurasa wake wa Twitter na kueleza kuwa serikali imeelekeza nguvu zake zote kuwaokoa manusura waliofukiwa na kifusi huku akiwataka waliowapoteza ndugu zao kwenye tukio hilo kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu.Toa comment