local

Chatu Aliyeonekana Chato Achukuliwa – Pichaz

By

on

Chatu Aliyeonekana Chato Achukuliwa – Pichaz

NYOKA mkubwa aina ya chatu ambaye hivi karibuni alizua gumzo baada ya kuonekana Kitongoji cha Iseni, Kijiji cha Kijiji cha Kasala Kata ya Makurugusi wilayani Chato Mkoani Geita amechukuliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) na kumpeleka pori la akiba la Kigosi Mulowosi, lililopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

 

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Richard Bagolele amesema nyoka huyo anapelekwa pori la akiba la Kigosi kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Nyoka huyo aliyeanza kuonekana siku saba zilizopita aligeuka kivutio kwa wananchi waliodai kuwa ni baraka, wengi kushinda porini wakimtazama huku wakiwa na mbuzi, maji na unga na vyakula wakiamini endapo nyoka atakula watapata baraka ya mvua, kuongezeka kwa mavuno na kuondoa mikosi kijijini hapo hivyo kuwaletea mafanikio.

 

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amewataka wanakijiji wa kijiji cha Makurugusi waliokuwa wamepiga kambi porini wakisubiri maajabu ya nyoka huyo, wafanye kazi kwa bidii na kuachana na imani potofu za kupata baraka kwa matambiko na kuabudu nyoka na vitu vingine.

Loading…

Toa comment

Posted from

About erick

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *