Mbelgiji aamua kufunguka ukweli wake

KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems amesema kuwa bado nyota wake wanateswa na matokeo ya Ligi ya Mabingwa kwa kuwa tu hayakuwa matarajio yao wengi akili zao walielekeza zaidi huko ndiyo maana kwa sasa wanashindwa kuwa imara na kujiamini.

 

Simba ilitolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwezi uliopita dhidi ya UD Songo ukiwa ni mchezo wa awali kabisa wa michuano hiyo. Msimu uliopita Simba kimataifa ikiwa na kocha huyo walifika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika.

 

“Nikwambie ukweli nawaona kabisa wachezaji wangu wengi hawako sawa kabisa kisaikolojia na ukitaka kuona hilo ule mchezo na JKT walicheza kama basi tu na hii ni kutokana na kile ambacho walikipoteza. “Wachezaji wangu wengi walikuwa wana mipango yao na matarajio ya kimataifa, lakini kama
hivyo ikawa ghafla wametoka kama unavyojua mambo ya mpira yalivyo.

 

“Kwa sasa naona kabisa bado hawajarudi kwenye mstari hivyo wanatakiwa kutulia na kusahau yaliyopita na kukubali hali halisi kwa kilichotokea maana bila hivyo mambo yatakuwa sio mazuri,” alisema Aussems.

Toa comment