PEPE AITOSA IVORY COAST

STRAIKA wa Arsenal, Nicolas Pepe inasemekana ameachana na Ivory Coast ili kujiweka fiti katika klabu yake. Pepe sasa ina maana hatachezea Ivory Coast kwenye mechi zake za kirafiki.

 

Staa huyo inasemekana alichukuliwa vipimo na ilibainika alikuwa na tatizo dogo tu. Uongozi wa Arsenal, hata hivyo, uliomba Pepe arudi klabuni ili ajifue na klabu yake kujiandaa na mechi za Ligi Kuu England.

 

Arsenal inaona kuwa staa huyo bado hayupo fiti kutokana na ukweli kuwa alichelewa kuripoti kambini kutokana na kuichezea Ivory Coast katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zilizofanyika Julai nchini Misri.

 

Pepe ameanza kuichezea Arsenal, ambayo alijiunga nayo msimu huu akitokea Lille ya Ufaransa. Arsenal ilivunja rekodi yao ya usajili kwa kutoa kitita cha pauni milioni 72, ambayo ni rekodi ya usajili kwa klabu hiyo.

Toa comment