JOB OPPORTUNITIES

Majina ya Walioitwa Kwenye Usaili Tarehe 20 – 3 Octoba UTUMISHI (MWEKA,MDAs & LGAs, MSD, ATC, TCAA. TPA & CAMARTEC )

By

on


JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.NaEA.7/96/01/K/76 13 SEPTEMBA, 2019

TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs, College of African Wildlife Management (MWEKA), Marine Services Company Limited, Medical Stores Department (MSD) Arusha Technical College (ATC), Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA), Tanzania Ports Authority (TPA) na CAMARTEC anapenda kuwataarifu waombaji kazi waliotuma maombi ya kujaza nafasi wazi katika ofisi mbalimbali za Umma kama zilivyoainishwa kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 20 SEPTEMBA, 2019 hadi 3 OKTOBA, 2019 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu saili hizo. Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-

i. Usaili utafanyika kuanzia tarehe 20 SEPTEMBA, 2019 hadi 3 OKTOBA, 2019
kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili.
ii. Muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
iii. Kila msailiwa anatakiwa kukumbuka (Serial Number) yenye jina lake kama ilivyotoka kwenye tangazo hili pamoja na eneo la chumba cha usaili wa mchujo, kwakuwa Wasailiwa wote hamruhusiwi kuja/kuingia na simu wala kifaa chochote cha kunakili taarifa au matukio katika chumba cha usaili;
iv. Kila msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
v. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi,
Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
vi. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha
kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, StashahadayaJuu, Shahada
nakuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
vii. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”,
“Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form IV and
form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA
KUENDELEA NA USAILI;
viii. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;
ix. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
x. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU na NECTA); na
xi. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili
watambue kuwahawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi
za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya Tangazo husika.
xii. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma
wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za
kufanyia kazi.

Kusoma majina hayo pakua PDF HIYO HAPO CHINISource link

About erick

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *