local

Rais Magufuli awatumia Sauti Sol kufikisha ujumbe kwa wanaokwamisha maendeleo ya nchi ‘Walioikamata ndege yetu, Ni wivu tu’ (+video)

By

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa sababu ya ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kukamatwa nchini Afrika Kusini ni wivu, Hii ni kutokana na shirika hilo kuanza kuimarika kwa kuteka soko la ndani kwa asilimia 75.

 

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Septemba 16, 2019 alipokuwa akizindua kituo cha mfumo wa rada ya kuongozea ndege katika kituo cha Dar es Salaam, Ambayo ni moja ya rada mpya nne zitakazofungwa nchini na kuwezesha kuongoza ndege katika anga lote la Tanzania.

Akikazia sakata la kukamatwa kwa ndege hiyo nchini Afrika Kusini, Rais Magufuli amesema kuwa licha ya kukamatwa kwa ndege hiyo ambayo tayari imeshaachiwa. Yeye ataendelea kuchapaka kazi, huku akitolea mfano kutoka kwenye mashairi ya wimbo wa Extravaganza wa kundi la Sauti Sol kutoka Kenya.

Rais Magufuli ametumia mashairi hayo yanayosema, “Wakifunika, tunafua, wakianika, tunaanua, wakitufungia milango, wanatukuta ndani.”.

Akitolea mfano kupitia mashairi hayo, Rais Magufuli amesema kuwa watu wanaokwamisha maendeleo ya nchi kamwe hawawezi kumsumbua yeye na Watanzania wanaopenda maendeleo na kuhimiza Wananchi kuchapa kazi kwa bidii na kupenda vitu vyao.

Posted from

About erick

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *