local

Siku za Gareth Bale ndani ya Real Madrid zahisabika

By

on

Inadaiwa mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale amechoshwa na maisha ya klabu na sasa anachohitaji ni kuondoka hii ni kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo nchini Hispania Guillem Balague alipofanya mazungumzo yake na BBC Radio 5 Live.

Bale alitarajiwa kujiunga na klabu ya ligi kuu ya Uchina Jiangsu Suning kwa mkataba wa miaka mitatu majira ya joto akitarajiwa kulipwa £1m kwa wiki – lakini Real ilikatiza makubaliano hayo kwasababu waliitisha ada ya uhamisho.

Mnamo Julai, meneja wa Real, Zinedine Zidane amesema wanatarajia kuondoka siku za hivi karibuni kauli ambayo wakala wa Bale, Jonathan Barnett alijibu kuwa: “Zidane ni aibu tupu – hana heshima kwa mchezaji ambaye amejitolea sana kwa Real Madrid.”

Bale ameshinda mataji manne ya ubingwa wa Ulaya, taji moja la ligi ya Uhispnania, la Copa del Rey na matatu ya Uefa Super Cups na Club World Cups akiwa Real, na amefunga zaidi ya magoli 100.

Baada ya kutibuka kwa makubaliano ya uhamisho wake kwenda China, mchezaji huyo wa kimataifa wa wales alijitoa katika mechi ya kabla kuanza kwa msimu huko Munich – hatua iliyoelezwa kwamba hayupo sawa kimawazo kuweza kucheza.

Lakini aliachwa nje ya kikosi kilichocheza wiki iliyopita katika mechi ya Champions League dhidi ya Club Bruges, kabla ya kurudi katika kikosi cha kwanza kwenye mechi waliopata ushindi wa 4-2 dhidi ya Granada Jumamosi.

“Gareth Bale amechoshwa,” anasema Balague. “Hawezi tena kuendelea. Katika wakati ambapo alikuwa aking’ara, akijua kila anapocheza anazidi kuimarika, ghafla ameishia kutazama mechi kutoka nje ya uwanja dhidi ya Bruges. Hakuna ajuae kwanini.

“Ana hasira, amechanginiyika. Zidane aliporudi katika klabu aliamua hamtaki Bale, pasi kutolewa ufafanuzi wa wazi wa kwanini.

“Bale aliambiwa kuwa Zidane, ambaye amekuwa na uhusiano wa kikazi naye, alifanya uamuzi kuwa anajitayarisha kwa kuondoka kwake.

“Wakala wake, Jonathan Barnett, alikwenda kumtafutia nafasi nyingine, lakini Bale alipendelea kuliko uamuzi mwingine wowote kusalia katika klabu hiyo.

“jambo ambalo mchezaji huyo haelewi ni kwanini milango ilifunguliwa, alafu kwanini kwanini hawakumruhusu kuondoka. Madrid ilikubali kutotoza ada klabu ya Uchina Jiangsu Suning, lakini hatimaye walibadili uamuzi huo kwasbabau waliamini timu hiyo ya Uchina ipo tayari kulipa kitita kikubwa kumpata James Rodriguez, uvumi ulioishia kuwa uongo.

“Bale amecheza vizuri katika wiki za hivi karibuin – kwa kiasi fulani ni kutokana na hasira – kufuatia pengo na na namna kocha huyo anavyomchukulia, na hatimaye ameamua kukaidi.

“Uamuzi wa kumtomshirikisha katika mechi dhidi ya Bruges ni mgumu kuuelewa, na imekuwa kama hatua ya mwisho.

“Kwa mara ya kwanza tangu awasili Real Madrid msimu wa joto mnamo 2013, mchezaji huyo anataka kuondoka. Anahisi kwamba anayotendewa sio sawa.”

Posted from

About erick

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *