local

Wasomaji Tandale Uzuri Wasema Betika Haliwapiti

By

on

Wasomaji Tandale Uzuri Wasema Betika Haliwapiti

 

MAPEMA leo Jumatano, timu ya maofisa masoko ya Global Publishershers imetembelea maeneo ya Tandale Uzuri, Kigogo Freshi na maeneo mengine ya Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuendelea kulitangaza zaidi Gazeti la Betika ambapo baadhi ya wasomaji wameelezea furaha yao kuwa kila linapotoka Siku ya Jumatano huwa hawalikoso kutokana na umuhimu wa gazeti hilo hususani kwenye masuala ya kubeti.

Betika ambalo hutolewa bure kwa wenye umri kuanzia miaka 18, linachapishwa na Kampuni ya Global Publishers na huingia mtaani kila Jumatano.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi linalojihusisha na masuala ya betting na lotto, lina takwimu za ligi tofauti na matangazo mbalimbali ya biashara.

Baadhi ya wasomaji waliokutana na timu ya maofisa masoko ya Global Publishers, walizidi kulisifia gazeti hilo kuwa gumzo kila kona ya nchi na kurahisisha kwenye masuala ya michezo ya kubeti.

Gazeti hilo heshima yake imeendelea kukua siku hadi siku na sasa lina watangazaji wengi ambao wanatangaza biashara zao kupitia Betika kwa bei nafuu.

Wote wanaofanya kazi na Betika wanapata ofa ya kutangaziwa biashara zao kwenye mitandao ya kijamii ya Kampuni ya Global Publishers katika Instagram, Facebook, Twitter na Global TV Online.

Loading…

Toa comment

Posted from

About erick

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *