Breaking: Stars Yatinga Cameroon CHAN Yapindua Meza Sudani

DITRAM Nchimbi na Erasto Nyoni leo wameamsha dude nchini Sudan kwa kuacha maumivu kwa timu ya Sudan wakiwa ugenini kwenye mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya kufuzu michuano ya Chan.

 

Stars ilikuwa inahitaji ushindi wa mabao 2 kutokana na kufungwa bao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uwanja wa nyumbani.

Stars ilianza kwa kushambulia mwisho wa siku ilipoteza kwa kufungwa bao la mapema lililowapoteza kiani Stars kabla ya kurejea kwenye ubora kipindi cha pili.

Erasto Nyoni ameonyesha ukomavu leo bila uwepo wa rafiki yake Kelvin Yondan ambaye ni majeruhi alipachika mbao wa kideo kabla ya Nchimbi kumalizia bao la pili la ushindi.

Toa comment