Karia: Tunaweka Historia Nyingine Sudan

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema kuwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, itaweka rekodi ya kuifunga tena Sudan ikiwa kwao kama ilivyofanya mwaka 2009 na kufuzu CHAN. Tanzania na Sudan zitacheza leo mchezo wa pili wa kufuzu CHAN, ambapo katika mchezo wa kwanza Tanzania ilifungwa bao 1-0 ikiwa nyumbani jijini Dar.

 

Karia ameliambia Championi Ijumaa kuwa malengo ya timu ni kuhakikisha wanapata matokeo
mazuri ugenini kama walivyofanya mwaka 2009, hivyo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanafuzu kwa kupata ushindi mzuri.

 

“Watanzania wote tunatamani tushinde mechi hii ili tufuzu CHAN, tutafanya kila kitu tupate matokeo ugenini kama tulivyoshinda 2-1 tukiwa kwao mwaka 2009, natumaini na kesho (leo) tutashinda tena,” alisema Karia.

 

Katika hatua nyingine, Karia amepokea jumla ya mipira 100 kutoka kwa Azim Khan ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Ligi na mmiliki wa timu ya Dar City ambaye amejitolea kwa ajili ya timu za Ligi Daraja la Kwanza na la pili ambao kila timu itapata mipira miwili.

Toa comment