local

Ighalo ashindwa kusafiri na Manchester United kisa virusi vya Corona

By

on

Mshambuliaji wa Manchester United Odion Ighalo atakosa mazoezi na klabu hiyo nchini Uhispania kutokana na hofu kwamba virusi vya corona vinaweza kumzuia kuruhusiwa kuingia nchini Uingereza .

Ighalo mwenye umri wa miaka 30, alisafiri kuelekea mjini Manchester kutoka China wikendi iliopita baada ya kutia saini kandarasi ya mkopo kutoka klabu ya Shenghai Shenhua.

”Angependelea kujiunga na wachezaji wengine ili kuweza kujuana”, alisema Mkufunzi Ole Gunnar Solskjare akizungumza na runinga ya MUTV.

”Lakini hatari ya masharti ya mpakani, hatutaki kuhatarisha”.

Wakati huohuo kiungo wa kati wa Man United Scott McTominay na beki Axel Tuanzebe ambao wote wamekuwa na majeraha ya muda mrefu watasafiri kuelekea Uhispania.

United hawatarudi hadi siku ya Ijumaa kabla ya mechi yao ya ligi ya Uingereza dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge tarehe 17 February.

By Ally Juma.

Posted from

About erick

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *