NABII Aliyemtabiria JPM Urais Atabiri Rais Mpya Burundi – Video

Kiongozi wa Kanisa la Ufunuo lililopo Kimara Bonyokwa Jijini Dar, Askofu Paul Bendera amezidi kuendeleza kazi yake ya utume na kupandikiza mbegu ya imani kwa mataifa na sasa ametua nchini Burundi ambako amefanya maombi makubwa ya kuimarisha amani nchini humo.

 

Askofu Bendera ambaye amekuwa mbeba maono ya Mungu amemtabiria mteule wa kuwania urais kupitia chama cha CNDD-FDD, Jenerali Evariste Ndayishimiye kuwa atashinda na kuwa Rais ajaye wa Burundi.

 

Pia amemshukuru Rais wa sasa wan chi hiyo, Piere nkurunzinza kwa moyo wake wa uzalendo na mambo mazuri mengi aliyoitendea nchi hiyo katika kipindi chote cha uongozi wake.

 

Askofu Bendera amemshukuru pia Rais wa Tanzania, Dkt. John pombe Magufuli kwa kuweka misingi imara ya ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi na kwamba heshima zote wanazopewa wachungaji wa Tanzania wanapofika Burundi na nchi nyingine basi zianzie kwa Rais Magufuli mwenyewe.
Toa comment