local

Nzige kusababisha njaa Afrika Mashariki, Waziri mkuu aeleza Serikali ilivyojipanga “Wakishambulia kwa nusu saa hupoteza tani 80 za chakula” – Video

By

on

Kanda ya Afrika Mashariki inaweza kukumbwa na njaa kama wimbi la nzige wanaokula mimea kwa haraka na malisho ya mifugo hawatadhibitiwa, afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa alisema.

Itasababisha mzozo wa chakula, Dominique Burgeon, mkurugenzi wa shughuli za dharura wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa(FAO), amesema. Ethiopia, Somalia, Kenya, Tanzania na Uganda zimeathiriwa na nzige.

Juhudi za kudhibiti wadudu hao hadi sasa hazijafanikiwa.

Unyunyiziaji wa dawa ya kuua wadudu ndio njia bora zaidi ya kukabiliana na nzige lakini nchi katika kanda hiyo hazina raslimali zinazofaa kukabiliana nao.

Kuna hofu kwamba nzige – ambao tayari wamefikia mabilioni wanaweza kuongezeka zaidi.

NzigeNzige hao wamesambaa kuanzia Yemen hadi maeneo mengine ya Bahari ya Shamu.

Kwa mujibu wa BBC. Shirika la chakula FAO linasema wadudu hao wanazaliana haraka sana kiasi kwamba idadi yao inaweza kuongezeka mara 500 kufikia mwezi Juni.

Umoja wa mataifa sasa unaitolea wito Jamii ya kimataifa itoe takriban dola milioni 76 kudhamini usambazaji wa dawa katika maeneo yaliyoathiriwa.

” Kama haitafanya hivyo, hali itakua mbaya zaidi, halafu mtahitaji kutoa msaada mkubwa wa chakula kwa ajili ya hali ya kibinadamu hali ambayo inaweza kudhibitiwa ,” Bwana Burgeon amesema

Locusts on a tree

Somalia imetangaza hali ya dharura kufuatia mzozo wa nzige. Serikali ya Ethiopian imetoa wito wa kuchukuliwa kwa “hatua za mara moja” za kukabiliana na tatizo la nzige ambao wamevamia majimbo manne kati ya tisa ya nchi hiyo.

Kenya imetuma ndege kunyunyiza dawa katika mikoa kadhaa, huku Uganda ikipanga kutuma wanajeshi katika mikoa ya kaskazini mwa nchi hiyo kunyunyiza dawa ya kuua wadudu hao katika maeneo yaliyoathiriwa.

Nzige hao wanaaminiwa kutoka katika nchi ya Yemen miezi mitatu iliyopita. Uvamizi wa nzige ni mbaya kuwahi kushuhudiwa nchini Kenya kwa miaka 70 na mbaya kuwahi kushuhudiwa nchini Ethiopia kwa miaka 25.

Mbali na hilo Waziri mkuu wa Tanzania Mh. Kassimu Mjaliwa ameeleza jinsi serikali ya Tanzania ilivyojipanga kukabiliana na wadudu hawa aina ya nzige ambao kwa sasa wameharibia ekari nyingi za mazao nchini Kenya. “Wakivamia shamba kwa nusu saa huharibu tani 80 za chakula.”

By Ally Juma.

Posted from

About erick

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *