StarTimes Yazindua Tamthilia Mpya – Video

KAMPUNI ya Star Media, kupitia king’amuzi chake cha StarTimes, imezindua tamthilia mpya ya Razia Sultan, ambayo imekuja baada tu ya Tamthilia ya Waaris kujizolea umaarufu mkubwa kupitia chaneli yao ya St Swahili.

 

StarTimes imezindua tamthilia hiyo ikiwa ni mahususi kwa ajili ya msimu huu wa wapendanao kwa kuamini kuwa mara baada ya kuanza kuruka rasmi itawavutia na kujizolea umaarufu kwa watazamaji wote waliokuwa wakiifuatilia Waaris.

 

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Meneja Masoko wa StarTimes, David Malisa alisema, tamthilia hiyo

ya Razia Sultan, inamhusu mwanamke machachari aitwaye Razia Sultan ambaye ndiye mhusika mkuu na mtawala wa kike wa Delhi Sultanate.

“StarTimes hapo tu kwenye mambo ya tamthilia sio mwisho, kwani tuna maudhui mbalimbali ikiwemo katuni za watoto, Ligi za Bundesliga, Euro 2020, Kombe la FA na nyingine nyingi.

 

“Pia kwa kuwajali zaidi wateja wetu, tumepunguza gharama za dekoda ya dish kutoka Sh 99,000 ya awali mpaka Sh 76,000, hivyo utaona kuwa haya ni mahaba ya ajabu kabisa na kwamba StarTimes itaendelea kuwapenda na kuwaheshimu wateja wake siku zote.

 

“Hebu jiunge sasa kwa kulipia king’amuzi chako kwa Sh 18,000 kwa kifurushi cha antena na Sh 21,000 kwa watumiaji wa dishi,” alisema Malisa.
Toa comment