Rc Makonda aruhusu boda Boda na Bajaji kuingia mjini

Mkuu Wa Mkoa Wa Dar es Salaam Poul Makonda ameruhusu madereva Wa Boda Boda na Bajaji kuingi mjini ili kuweza kusaidia changamoto ya usafiri Kutokana na ugonjwa Wa korona. Akizungumza na global publishers alipokiwa kituo cha daladala cha Makumbusho alisema kuwa kuanzia leo boda boda kuingia mjini kwa sababu Ku tokana na ugonjwa Wa Corona daladala zinatakiwa kupakia leval siti.

“Kuanzia Leo bodaboda au bajaji akipata abiria anaruhusiwa kuingia mjini mpaka hapo changamoto ya ugonjwa itakapoisha.

“Pia kuanzia kesho saa sita mchana gari zitakuwa zinatembelea ruti fupi na abiria wawe lever siti na siyo abiria akishaona gari imeshajaa asiingie maana kuna mwingine anaingia alafu anakaa katikati chini siyo kwenye viti.

Nimeshawaomba wenye nyumba kupunguza kodi ya asilimia hamsini Ku tokana na ugonjwa huu.
“Ndege moja ya Ethiopia inaingia kwa ajili ya watanzania ambao wanahitaji kurudi nyumbani,sasa wakishaingia watafikia karantini kwa ajili ya uangalizi kwa hiyo mtu yeyote asiende Uwanja Wa Ndege atapikelewa na ofisi ya Mkoa na kupelekwa Karantini kwa siku 14.

“Mwananchi unapoona dalili usinywe dawa na unaenda hospital,na bahati nzuri dalili zinajulikana ukiona unazo jitenge na wapendwa wako na piga namba za msaada usaidiwe.

“Nawaomba wazazi kipindi hiki watoto wapo nyumbani wasiende kwenye mabaa na kupata ugonjwa na kuurudisha nyumbani ni vyema tukatulia nyumbani Kama hakuna ulazima Wa kutoka.
“Mungu akipenda tutakuwa na helkopta zitapita kumwaga dawa za kuua wadudu na gari pia zitapita kila sehemu nitatumia mamlaka yangu kufanya kazi alizonitumza Rais John Pombe Magufuli,”alisema Makonda.

Stori:Neema Adrian
Toa comment