Sallam Kuukataa Mkono wa Harmonize Msibani, Chanzo ni Hiki?

Meneja wa WCB Sallam Sk pamoja na msanii Harmonize ambaye aliwahi kuwa chini ya lebo hiyo ya WCB wameingia kwenye headlines baada ya Sallam kugoma kupokea mkono wa salamu wa Harmonize katika msiba wa aliyekuwa mke wa Hamis Taletale (Babu tale).

Tukio hilo lililotokea msibani limeacha maswali mengi kwa baadhi ya watu walioshuhudia kitendo hicho, na kuhoji tatizo kati ya hawa ‘Mabwana’ ni nini hasa mpaka kufikia Sallam kumuonyesha Harmonize chuki ya wazi wazi mbele ya watu.

Harmonize alisainiwa WCB, lebo ambayo inamilikiwa na msanii Diamond Platnumz  mwaka 2015 na kutambulishwa rasmi na ngoma ya ‘Aiyola’ ambayo ilifanya vizuri na kumuweka kwenye ramani ya muziki wa Tanzania, Afrika na dunia kiujumla na baada ya hapo zikafata ngoma nyingi ambazo zote zilifanya vizuri, chini ya usimamizi wa Lebo hiyo ambayo inasimamiwa na mameneja kadhaa akiwemo Sallam Sk, Babutale, Mkubwa Fela. Baada ya kudumu wa takribani miaka minne yenye mafanikio katika lebo hiyo, Harmonize alitangaza kujitoa kwenye lebo hiyo mwaka jana 2019, na kueleza sababu kadhaa zilizomsukuma kuondoka katika lebo hiyo.

Kitendo chake cha kuondoka WCB, kilileta ushindani mpya kwenye game ya muziki wa Bongofleva, Harmonize akaanzisha lebo yake, Konde Music Woldwide maarufu kama Konde Gang ambayo inashindanishwa sana na WCB (Lebo yake ya zamani).

Katika ushindani huo mpya ulioibuka kati ya Harmonize na Diamond Platnumz, hakukuwa na ‘Bifu’ la wazi wazi lililowahi kuonekana kati ya Harmonize na Diamond, au Harmonize na uongozi wa WCB hali inayofanya watu wajiulize maswali mengi , ‘Kuna nini kati ya Harmonize na Sallam?’

Tujikumbushe

Mapema waka huu February 9, Harmonize alipost kipande cha video kwenye kurasa yake ya instagram akiwa anapromote video yake mpya ya Singeli ‘Hajanikomoa’ na kuandika maneno ” Kwa Haraka Haraka Nikajua Boss Wangu Wa Zamani….!!!!! 🤔🤔 Duniani Wawili Wawili Jamani…!!!! 🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Na Anavopendaga Kupati Yani Niyeye Kabisa….!!!! 😇😇” 

 

Kitendo cha Harmonize kuandika  ‘Boss wangu wa Zamani’ kiliwaaminisha watu kuwa alimlenga Sallam SK moja kwa moja. Je Unahisi ‘Bifu’ lilianzia hapa?
Toa comment