NEWS

DILI LA KASEKE YANGA LIMEIVA

By

on


NA JESSCA NANGAWE

UBORA wa winga wa Yanga, Deus Kaseke, umeendelea kumuweka kwenye viwango vya juu na sasa mabosi wa klabu hiyo hawana mashaka yoyote juu ya kumuongezea mkataba wa kuwatumikia tena Wana Jangwani. Kaseka tangu arejee Yanga akitokea Singida United, amekuwa msaada mkubwa kwa timu yake akicheza kwa mafanikio na kuchangia ushindi katika mechi mbalimbali.

Licha ya mkataba wake kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu, habari za ndani kutoka klabuni hapo zimesema tayari winga huyo ameandaliwa kandarasi nyingine anayotarajia kuisaini wakati wowote kuanzia sasa. Kocha wake, Luc Eymael, ameendeela kumtumia mara nyingi katika kikosi cha kwanza huku akifanya vyema, hivyo kuwa miongoni mwa nyota tegemeo ndani ya kikosi hicho kwa siku za hivi karibuni.

“Wapo wachezaji ambao mikataba yao ipo ukingoni kumalizika, si yeye peke yake, kwasasa wanaandaliwa mingine akiwemo Kaseke, tunataka Yanga mpya na ya tofauti msimu ujao, tunaandaa wachezaji ambao wataiweka Yanga katika ramani nyingine ya soka itakayoendana na falsafa yetu ya mabadiliko,” kilisema chanzo hicho.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Ndanda, Kaseke aliweza kuing’arisha Yanga na kupata ushindi wa mabao 3-2 iliyowawezesha kuondoka na alama tatu huku ikipanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.Source link

About erick

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *