local

Ndinga Ya Jishindie Gari Na Championi Kutolewa Leo

By

onNdinga Ya Jishindie Gari Na Championi Kutolewa Leo

DROO kubwa ya bahati nasibu ya Jishindie Gari na Championi hatimaye imefikia ukomo wake na leo Jumatano droo hiyo inatarajiwa kufanyika kwenye ofisi za Global publishers zilizopo Sinza Mori jijini Dar.

 

Bahati nasibu hiyo ya Baba Lao inakwenda kutamatishwa baada ya kudumu kwa zaidi ya miezi mitatu na ilitakuwa kumalizika mapema mwezi uliopita ili ilishindikana kutokana na shughuli nyingi kusimama kutokana na uwepo wa janga la Corona.

Bahati nasibu hiyo ilianzishwa kwa lengo la kurudisha kidogo kinachopatikana kwa jamii ambayo imekuwa ikiyasapoti magazeti ya Championi na Global Publishers kwa ujumla wake, kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

 

Mkuu wa Idara ya Usambazaji wa Global Publishers, Anthony Adam amesema kila kitu kuhusu kuchezeshwa kwa droo hiyo kimekaa vizuri na wasomaji wote wa Championi ambao walishirikli bahati nasibu hiyo wakae jirani na simu zao kwani lolote linaweza kutokea.

Droo hiyo kubwa itafanyika na kurushwa moja kwa moja kupitia Global TV Online huku taarifa za mshindi atakayepatikana zitasikika kupitia spika za +255Global Radio, TBC Taifa na Channel 10.

 

“Nafikiri kila mtu yupo tayari kusikia akitajwa kuwa mshindi wa gari mpya aina ya Toyota FunCargo, sisi kama viongozi tumekamilisha kwa upande wetu maandalizi ya droo hii, kilichobakia ni kujua nani anakwenda kuwa mshindi wetu.

“Nirudie kusema kuwa bahati nasibu hii itakuwa ni ya ukweli na uwazi, itarushwa moja kwa moja kupitia Global Tv Online, lakini pia itaonekana kupitia TBC na Channel 10, bila kusahau wasisimamizi wa michezo ya kubahatisha nao watakuwepo.

“Tunamtakia kila la kheri mshindi ambaye atapatikana kwa kuwa amesubiriwa kwa muda wa zaidi ya miezi mitatu kutimiza ndoto zake, matarajio yetu kuwa mshindi huyo atakayeondoka na gari atakwenda kubadilisha maisha yake kama ilivyo lengo la bahati nasibu hii,” alisemaAnthony.

Idara ya Masoko na Usambazaji ya Global Publishers, katika kukamilsha ambapo washindi wote walijinyakulia zawadi mbalimbali kama vile fedha shilingi elfu kwa washindi 12, huku washindi watatu wakiondoka na simu janja.

JINSI YA KUSHIRIKI

Nunua Gazeti la Championi kisha fungua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya kushiriki bahati nasibu hiyo. Jaza kuponi kama maelekezo yalivyo.JINSI YA KUTUMA:Mpe kuponi yako muuza magazeti aliye karibu nawe popote ulipo, au peleka kwenye Ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Mori, Dar, au tuma kwa njia ya barua, Jishindie Gari, Global Publishers, S.L.P 7534, Dar es Salaam.

MASHARTI YA KUSHIRIKI:Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd na watoto chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kushiriki bahati nasibu hii.Kuponi zitumwe kutoka nakala halisi ya gazeti, vivuli (fotokopi) haviruhusiwi.

Mtu anaruhusiwa kutuma kuponi nyingi kadiri awezavyo ili ajiongezee nafasi ya kushinda. Kuponi zote zitachezeshwa kwenye droo ya awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu.

ISSA LIPONDA, Dar es SalaamToa comment

Posted from

About erick

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *