NEWS

SIMBA JEURI AZAM KIBURI – Gazeti la Dimba

By

on


NA JESSCA NANGAWE

NI mechi ya wababe wawili, mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba dhidi ya Azam FC, wanaotarajia kuonyesha umwamba katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa Wekundu hao wa Msimbazi tangu walipokipiga na Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu Bara ulioitangazia ubingwa wiki iliyopita jijini Mbeya.

Katika mchezo wa leo, timu zote zitaingia uwajani zikiwa na shauku ya ushindi ambapo Simba watataka kiuendeleza ubabe na pia kulinda hadhi ya kuwa mabingwa wa soka nchini, huku Azam FC nao wakitaka kutibua rekodi ya Simba na pia kulipa kisasi. Kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, amesema baada ya kunyakua taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/20 nguvu zao wanaelekeza katika michuano hiyo ya FA. Sven alisema wachezaji wote wako fiti tayari kuipigania timu yao katika michuano ya FA ingawa amekiri mchezo huo utakuwa mgumu. “Ilikuwa safari ndefu hadi kujihakikishia ubingwa, kimahesabu hakukuwa na mechi rahisi, katika mechi dhidi ya Prisons lengo letu lilikuwa tupate hata pointi moja na tumefanikiwa sasa tunahamishia malengo kwenye michuano ya FA,” alisema. Kwa upande wa Azam FC, kocha mkuu Aristica Cioaba alisema, mchezo wa leo kwao utakuwa mgumu ukizingatia wapinzani wao wametoka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, lakini watapambana kwa nguvu zote ili kupata matokeo mazuri. “Tunatambua uwezo wa wapinzani wetu, tunakwenda kupambana kwa kuwa tumejipanga kutetea ubingwa wetu, tunajua tutakutana na upinzani mkubwa lakini hawawezi kututoa kwenye mipango yetu,” alisema Cioaba. Rekodi za timu hizi msimu huu zinaonyesha  Simba iliibuka na ushindi wa mabao  4-2 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii huku ukitoka kifua mbele katika mzunguko wa kwanza wa ligi kwa ushindi wa bao 1-0 kisha ikaibuka na ushindi wa mabao 3-2 kwenye mchezo wa marudiano. Katika mchezo wa nusu fainali Kombe la Mapinduzi, timu hizo zilitoka sare ya 0-0 ndani ya dakika tisini lakini Simba wakaibuka washindi kwa mikwaju ya penalti 3-2.Source link

About erick

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *