NEWS

YANGA IJAYO INAFURAHISHA – Gazeti la Dimba

By

on


NA JESSCA NANGAWE

YANGA hawaumizwi na ubingwa wa Simba kwani akili yao kwa sasa ni kutwaa ubingwa wa Kombe la FA sambamba na kusuka upya kikosi chao kitakachokuwa hatari msimu ujao.

Ikiwa kwenye mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji, Yanga imepania kuwa ya kisasa kila idara huku ikiweka nguvu zaidi katika maboresho ya kikosi hicho msimu ujao kwa kuboresha benchi la ufundi hadi wachezaji.

Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, klabu hiyo ina mipango mingi itakayoibadilisha kutoka ile iliyokuwepo hivi sasa na kuisogeza mbele, lengo likiwa ni kufanya vizuri katika michuano ya ndani vilevile ya kimataifa.

Mwakalebela alisema ili kuendana na kasi ya mabadiliko wamepanga kuwa na kikosi kipana ambacho kitakuwa cha ushindani zaidi na yote hayo yanaendelea kukamilika siku hadi siku.

“Kwasasa tunapambana kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa FA, na kitakachofuata ni kuangalia Yanga inahitaji mchezaji wa aina gani na benchi la ufundi likae vipi,” alisema Mwakalebela.

Alisema wamedhamiria kufanya tukio kubwa la utambulisho wa kikosi katika hafla ya Wiki ya Wananchi ambapo safari hii wamepanga kuacha historia.

Aidha Yanga imepania kufanya mabadiliko makubwa ndani ya benchi la ufundi kwa msaada wa Kampuni ya La Liga ambao wameahidi kuleta wakufunzi kutoka Hispania watakaorekebisha mambo mbalimbali watakayoona hayakukaa sawa.Source link

About erick

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *