MASHABIKI WA SIMBA WAMUONYESHA CHA MTEMA KUNI MAYELE…APEWA KIBAO CHA KUFA MTU…MASHABIKI wanaodhaniwa kuwa ni wa Simba juzi walijitokeza kwa wingi Bandari ya Dar es Salaam kuwapokea watani zao wa jadi, Yanga ambao waliwasili wakitokea Zanzibar, zaidi walionekana wakimganda straika Fiston Mayele na kupiga naye picha.

Yanga iliondoshwa katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa penalti 9-8 mbele ya Azam FC.

Majira ya saa saba, msafara wa Yanga ulishuka bandarini hapo ambapo walikutana na mashabiki wengi waliokuwa wamevalia jezi za Simba huku wakishangilia kwa mtindo anaotumiaga straika wa Yanga, Fiston Mayele inapotokea amefunga bao.

Mashabiki hao walisikika wakiimba: “Tunalitaka kombe letu, tunalitaka kombe letu.” Pia walipata muda wa kupiga picha na Mayele ambaye ni kinara wa utupiaji ndani ya Yanga kwenye ligi akiwa na mabao matano na pasi moja.

Hassan Bumbuli, Mkuu wa Kitengo cha Habari Yanga, alisema kuwa hesabu zao kwa sasa ni kwenye ligi.

“Bado tuna kazi ya kufanya hasa baada ya kushindwa kutwaa taji la Mapinduzi na malengo yetu ilikuwa ni kutetea ubingwa wetu, kilichotokea ni matokeo,” alisema Bumbuli.

Source link

About Author /

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Start typing and press Enter to search