SAA CHACHE BAADA YA KUTAMBULSIHWA SIMBA…CHAMA ARUSHA ‘KIJEMBE’ YANGA…MKATABA WAKE UKO HIVI…


Saa chache baada ya kutambulishwa kurudi Simba, Kiungo fundi wa mpira kutoka Zambia Clatous Chama amerusha kijembe kwenda kwa mashabiki wa timu pinzani kwa Simba, Haswa Yanga waliokuwa wakitaka kumsajili.

Kupitia ukurasa wake wa kijamii, Chama ameandika ujumbe huo unaosomeka kama “Mwenda kwao si Mtoro” , ujumbe ambao unaweza kumaanisha kuwa yupo sahihi kurudi kwenye timu hiyo iliyompa jina na mafanikio makubwa.

Aidha pia ujumbe huo unaweza kuwa ni kijembe kwa Yanga, ambao walihusishwa kumtaka kwa udi na uvumba kabla ya kuzidiwa kete na Simba ambao hawakutumia nguvu nyingi kumrudisha kiungo huyo anayeichezea pia timu ya Taifa ya Zambia.

Klabu ya Simba kupitia Msemaji wake, Ahmed Ally imesema kuwa Chama amerudi nyumbani ambapo amesaini mkataba wa miaka mitatu ya kucheza na Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mbali na Chama , Simba imesema kuwa itaendelea kutangaza wachezaji wapya waliosajiliwa kwenye dirisha hili dogo la usajili ambalo linafungwa leo Jumamosi.

Source link

About Author /

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Start typing and press Enter to search