Afisa Elimu Pwani Atoa Somo Kwa Wahitimu Victory Secondary

Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Pwani, Bi Hildergard Makundi akizungumza kwenye mahafali hayo.

“Nawapongeza kwa kuwa mfano wa shule bora mkoani Pwani kwa mchango wake kielimu kwa kuwa wanafunzi wengi waliotokea hapa wamekuwa wataalam wazuri walipoelekea”.

Hayo yamesemwa na Afisa Elimu Taaluma mkoa wa Pwani Hildergard Makundi aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 13 ya Shule ya Sekondari ya Victory iliyopo Mwandege mkoani Pwani yaliyofanyika Septemba 26 mwaka huu.

“Nawapongeza shule hii kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusimamia vizuri taaluma inayokidhi viwango na kupelekea kutoa kipaumbele kwenye masomo ya sayansi.

“Mmemuunga mkono Raisi wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwenye suala zima la elimu na ndio maana kama tulivyosikia mabadiliko makubwa ya ufaulu kwa watoto.

Sehemu ya wahitimu wakiwa kwenye mahafali hayo.

“Shule hii ni mfano wa kuigwa kwa kuwa wameajiri walimu walio na sifa na uwezo mkubwa ndio maana tumeona mabadiliko makubwa kila mwaka na kupata wataalam mbalimbali kutoka hapa.

“Kikubwa ninachotaka kuwaambia wanafunzi ambao mnatarajia kufanya mtihani wa taifa mkafuate kile ambacho walimu wamewafundisha.

“Kama tulivyoona hapa kuna walimu wamewafundisha somo zuri la ujasiriamali mmetengeneza sabuni za maji, mafuta, mapambo na dawa za kusafishia vyoo hivyo basi mnaporudi majumbani mkatengeneze na kuuza ili mkajiingizie kipato.”Alimaliza kusema afisa elimu huyo.
Toa comment