Aika, Nahreel Karantini Siku 14

MEMBA wawili wa Kruu ya Navy Kenzo, Aika Marealle na Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ wamejiweka karantini kwa siku 14 sasa kujikinga na maambuziki ya Virusi vya Corona vinavyosababisha Ugonjwa wa COVID-19.

 

Aika ameiambia OVER ZE WEEKEND kuwa, walivyosikia tu virusi hivyo vimeingia Bongo, waliamua kujiweka karantini kwa kujifungia ndani kwao na watoto wao wawili wa kiume, Gold na Jamaica.

 

“Tunaogopa sana ukizingatia tuna watoto wadogo, tumeamua kujifungia na hatutoki hadi tusikie janga hili (Virusi vya Corona) limepita,” alisema Aika ambaye kuna tetesi kuwa ana ujauzito mwingine wa mtoto wao wa tatu.

 
Toa comment