Ajuza wa miaka 95 apona Virusi vya Corona, Italia

24 0

Katika siku za hivi karibuni, Italia imekuwa na sababu kidogo za kuwa na matumaini.

Taifa hilo ndilo lilioathirika zaidi na virusi vya corona barani Ulaya na kufikia tarehe 23 mwezi Machi zaidi ya watu 6000 tayari walikuwa wameaga dunia, ikiwa ndio idadi ya juu zaidi duniani.

Hata hivyo matumaini miongoni mwa baadhi ya wagonjwa yameweza kufufua tamaa.

Hatua hiyo inajiri katika kisa cha Alma Clara Corsini, ajuza wa miaka 95 ambaye alifanikiwa kupona baada ya kulazwa na dalili za ugonjwa huo tarehe 5 mwezi Machi katika hospitali moja mkoani Modena kaskazini mwa Itali.

Kulingana na gazeti moja la eneo hilo La Gazzetta di Modena, afya ya Corsini imeimarika hali ya kwamba ametoka hospitalini na kwamba tayari amerudi katika nyumba yake ya wazee aliokuwa akiishi katika manispaa ya Fanano katika mkoa wa Modena.

”Ndio niko salama . Ni watu wazuri walionitibu vizuri na tayari wananipeleka nyumbani” , Corsini aliambia La Gazzetta di Modena akizungumzia kuhusu uangalizi aliopata katika hopsitali hiyo.

Gazeti hilo pia lilisema jinsi wataalam walivyosema kwamba Corsini alipona bila kutumia dawa za kukabiliana na virusi ambazo hupewa wagonjwa ili kuwasaidia kukabiliana na maambukizi.

Maeneo yaliathirika zaidiVifo vinavyotokana na janga la coronavirus vimepita vile vya China ambapo ndio chanzo cha ugonjwaVifo vinavyotokana na janga la coronavirus vimepita vile vya China ambapo ndio chanzo cha ugonjwa

Picha ya mwanamke huyo mzee pamoja na maafisa wa afya waliomtibu ilisambaa sana katika mitandao ya kijamii nchini humo.

Mkoa wa Modena upo katika jimbo la Romagna ambalo ndio jimbo la pili zaidi kuathiriwa na virusi vya corona baada ya Lombardy.

Emilia Romagna kulingana na data ya kila siku ilisajili zaidi ya visa 8500 na takriban vifo 900 tarehe 23 mwezi Machi.

Idadi kubwa ya vifo hukumba watu wenye zaidi ya umri wa miaka 70.

Italia, ikiwa na zaidi ya vifo 6000 , imeipiku China ambayo ilikuwa na vifo 3200 wiki iliopita kuwa taifa lenye idadi kubwa ya vifo duniani.

Hatahivyo idadi ya siku mbili zilizopita inaonesha kupungua kwa visa vya vifo na maambukizi.

Takwimu kama hizo na kisa cha Corsini zinawapatia matumaini makubwa raia wa Italia.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *