Akamatwa akipeleka sumu Ikulu – Marekani – Dar24

18 0

Maafisa wa uhamiaji nchini Marekani wameeleza kuwa mwanamke mmoja amekamatwa akishukiwa kutuma kifurushi kilicho na sumu aina ya ricin kwenda kwa Rais wa Marekani,Donald Trump.

Mwanamke huyo ambaye hajatajwa jina alikamatwa kwenye mpaka huko Buffalo, New York , akijaribu kuingia Marekani akitokea Canada, na anaripotiwa kukamatwa akiwa na silaha.

Kwa mujibu wa wapelelezi  Barua hiyo inayoshukiwa kuwa na sumu inaaminika kutoka nchini Canada na iligundulika wiki iliyopita kabla ya kufika ikulu ya Marekani.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la habari CNN limeeleza kuwa  mshukiwa huyo anashukiwa kuwa huenda alituma sumu hiyo pia huko Texas, kwenye gereza na ofisi ya maafisa wa polisi

Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), na maafisa wa ulinzi wa siri wanachunguza barua hiyo ilitumwa kutoka wapi na ikiwa kuna nyingine zilitumwa kupitia huduma za posta za Marekani.

 Serikali ya Trump bado haijasema chochote kuhusu ripoti hiyo.

Nitamshauri Rais avunje bunge- Jaji Maraga
Serikali: Zalisheni mbolea zenye viwango

Comments

comments

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *