Alichokisema Nandy Kuhusu Kuwa na Ujauzito wa Billnass

MSANII wa kike kwenye muziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka kuhusu madai ya kuwa na ujauzito wa Billnass baada ya kuonekana kula udongo kwenye mtandao wa Snapchat siku kadhaa zilizopita.

 

Akizungumzia hilo mbele ya waandishi wa habari Nandy amesema watu wanamsema ni mjamzito kwa sababu ya ongezeko la mabadiliko yake ya mwili wake ambayo yanasababishwa na ukuaji.

 

“Sina ujauzito wowote…Watu wanasema mimi ni mjamzito kwa sababu ya mabadiliko ya mwili wangu ambayo yanasababisha kukua haraka kama kunenepa, ukiangalia familia yetu wote wanamaumbo makubwa halafu ni wanene labda na mimi ndiyo nimefikia hatua ya kuwa hivyo,” amesema Nandy.

 

Billnass na Nandy tayari wameshavalishana pete ya uchumba na kinachosuburiwa kwa hamu kubwa kwa sasa ni ndoa kati yao.
Toa comment