Alikiba Ataja Sababu ya Dodo na So hot Kushutiwa Zanzibar – Video

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’ leo Juni 10, 2020 amefunguka sababu iliyopelekea wimbo wake wa dodo kufanya vizuri sokoni kuwa ni wimbo wenye mahadhi ambayo watu wengi walikuwa wakiyataka.

Akizungumza katika mahojiano maalumu yaliyofanyika katika kipindi cha Bongo 255  kinachoruka kupitia +255 Global radio msanii huyo alisema pia ametokea kuyapenda mazingira ya Zanzibar ndio maana hata video zake zote mbili (Dodo na So hot) aliamua kufanya kule.

 

“ Kitu ambacho kimefanya wimbo wa dodo kufanya vizuri ni kuhusu ala zake, jinsi nilivyoimba na mahadhi ya muziki ambao nimeufanya ni muziki ambao ulitakiwa utoke kwa kipindi kile, lakini pia video zote ya ‘dodo’ na ‘so hot’ nimefanyia Zanzibar kwa sababu ni sehemu nzuri, sehemu inayovutia lakini pia ni sehemu ambayo naweza kupata kitu chochote ninachokitaka, Zanzibar kuna mandhari nzuri, Hotel nzuri na vitu vingine vya kuvutia”, alisemaToa comment