Aliyesakwa Miaka 12 na FBI kwa Mauaji ya Watoto Wake Anaswa!

4 0Aliyesakwa Miaka 12 na FBI kwa Mauaji ya Watoto Wake Anaswa!

Dereva wa taxi, Yaser Abdel Said (63) aliyekua akisakwa na Shirika la Upelelezi la Marekani  (FBI) kwa tuhuma za mauaji ya mabinti zake wawili kwa miaka 12 kwa kuwapiga risasi amekamatwa baada ya kukimbilia mafichoni kwa miaka 12 iliyopita.

 

Waranti ya kumkamata Yaser Abdel mwaka 2008 baada ya kuwapiga risasi binti zake, Sarah Yaser Said, 17, na Amina Yaser Said, 18. Mshukiwa huyo ambaye ni mzaliwa wa Misri aliwekwa kwenye orodha ya FBI, ya watu 10 wanaotafutwa zaidi mwaka 2014. Yaser hivi karibuni atahamishwa Kaunti ya Dallas, ilisema taarifa iliyotolewa na Idara ya FBI Dallas.

Jopo kazi la uhalifu wa ghasia linaloongozwa na FBI mjini Dallas limekuwa likimtafuta kwa muda mrefu Yaser Abdel,” alisema ajenti maalum wa FBI Dallas, Matthew DeSarno.

 

Mama ya wasichana hao, Patricia Owens, amesema amefurahishwa na hatua ya kukamatwa kwake, na kuambia vyombo vya habari vya mji huo: “Sasa wasichana wanaweza kupumuzika kwa amani.”

 

Islam Said, mtoto wa kiume wa mshukiwa, na Yassim Said pamoja na ndugu mmoja wa mshukiwa walishitakiwa kwa kumficha jamaa huyo. Uchunguzi wa mauaji ulianzishwa Januari 1, 2008 baada ya Amina na Sarah kupatikana wakiwa wameuawa kwa kupigwa risasi.

 

Siku hiyo, mshukiwa aliwabeba kwenye taxi wasichana hao kwa kisingizio kwamba anaenda kuwanunulia chakula. FBI inasema aliwapeleka hadi Irving, Texas, ambako inadaiwa aliwapiga risasi wasichana hao ndani ya gari. Wote walifariki kutokana na majeraha kadhaa ya risasi.

Kabla ya vifo vyao, jamaa wa familia aliwaambia polisi kwamba mshukiwa alitishia “kumdhuru” Sarah kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye sio Muislamu, kwa mujibu wa kituo cha habari cha CBC. Mauaji ya mwanafamilia anayedhaniwa kufedhehesha jamaa zake wakati mwingine husemekana kuwa “mauaji ya heshima” – lakini wakosoaji wanapinga maana inayotolewa kwa mauaji kama hayo.

 

Idara ya polisi ya Irving ilifanya uchunguzi wa mauaji ya Amina na Sarah na, kufikia Januari 2, 2008 waranti ya kukamatwa kwa Yaser Abdel Said ilitolewa. Tangu wakati huo, mawakala wa FBI “wamekuwa wakipambana kuwatafutia haki Amina na Sarah”, Mkuu wa Idara ya polisi ya Irving Jeff Spivey, alisema.Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *