Amber Rutty, Mumewe, James Delicious Wahukumiwa Jela Miaka 5

MSANII Rutyfiya Abubakary maarufu kama ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake Said Bakary pamoja na mtuhumiwa mwenzao James Charles ‘James Delicious’ wamehukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kulipa faini ya ya Tsh milioni 11 ama kutumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia katika makosa matatu likiwemo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Hata hivyo washtakiwa hao, ambao walikuwa wakikabiliwa pia na makosa ya kusambaza video zenye maudhui ya ngono mitandaoni, wameshindwa kulipa faini hiyo na hivyo wamepelekwa gerezani.
Toa comment