Arsenal yajipima ubavu na Liver, United kutaka kumsajili Antoine Griezmann

1 0

Arsenal imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji wa Barcelona Antoine Griezmann, 29, baada ya Lionel Messi kuamua kusalia Nou Camp na hivyo kuujingiza katika kinyang’anyiro hicho mbele ya miamba ya soka England, Manchaster United na Liverpool ambazo zenyewe zimetolea macho saini ya nyota huyo (Mail)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara ,29, ametupilia mbali ripoti zinazomhusisha na kuihama klabu yake msimu huu, ingawa Mhispania huyo ameikuwa akiivutia Liverpool na Manchester United. (Manchester Evening)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara amepiga tetesi zizomhusu yeye kuihama klabu yake

Real Madrid bado imekataa kutoa mustakabali wa winga wa Wales Gareth Bale, 31 kuhusu kuondoka katika klabu hiyo msimu huu. (Sport-in Spanish)

Real Madrid bado imekataa kutoa mustakabali wa winga wa Wales Gareth Bale

Livepool imeiambia Barcelona itawagharimu pauni milioni 15 ikiwa wanataka kumsajili kiungo wa kati Georginio Wijnaldum. (Mirror)

Kocha wa Wales Ryan Giggs anaamini mlinzi Ethan Ampadu,19, ana uamuzi mkubwa wa kufanya kuhusu uwepo wake Chelsea.(Sky Sports)

Newcastle imeweka dau la pauni milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji Callum Wilson na wanataka kukamilisha mchakato kwa ajili ya kumnyakua mchezaji huyo, 28 anayekipiga katika klabu ya Bournemouth kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi ya primia mwishoni mwa juma lijalo dhidi ya West Ham (Sunderland Echo)Manchaster United, Arsenal na Liverpool wako kwenye maandalizi mapya ya kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji wa Barcelona Antoine Griezmann

Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anataka kurejea Juventus, ambayo ndio sababu hajatia saini mkataba mwingine Old Trafford huku mkataba wake wa sasa unakamilika mwaka 2021. (Tuttosport)

Mazungmzo kati ya Chelsea na Rennes kuhusu uhamisho wa mlinda mlango Msenegali Edouard Mendy, 29, yamefikia katika hatua muhimu. (Sun)Paul Pogba anataka kurejea Juventus

Wachezaji wa Barcelona Luis Suarez,33 na Arturo Vidal,33, wamefanya mazoezi kando na wenzao siku ya Jumamosi wakati wote wawili wakijiandaa kuondoka kwenye klabu hiyo kuelekea Juventus na Inter Milan. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Barcelona na Brazil Rafinha, 27, anatolewa macho na Leeds United. (Talksport)

Crystal Palace inamuweka mshambuliaji wa Sassuolo Jeremie Boga kuwa mbadala wa Wilfried Zaha ingawa Napoli, Rennes, Atalanta na Bayer Leverkusen pia zinamuhitaji mchezaji huyo, 23. (Sky Sports)

Bristol City imekubali masharti kumsajili Alfie Mawson kwa mkopo kutoka Fulham. (Football Insider)

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *