Asha Muhaji Azikwa Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Dar leo (Picha +Video)

10 0

Asha Muhaji Azikwa Makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Dar leo (Picha +Video)

Msemaji wa Simba SC, Haji Manara akitoa wasifu wa marehemu.

Mwili wa marehemu Asha Muhaji (50) ambaye Mhariri wa Magazeti ya michezo ya Kampuni ya Habari Cooparation, Dimba na Bingwa pia Afisa Habari wa timu ya Simba SC, leo Alhamisi umepumzishwa kwenye makaburi ya Mwinyimkuu, Magomeni Dar.

Shughuli za msiba huo zilifanyika nyumbani kwao Kijitonyama Dar na kuhudhuriwa na wanahabari na wadau mbalimbali wa michezo ambapo makundi mbalimbali yalitoa salam za rambirambi.

Mohammed Mharizo ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Habari Coopation, Bingwa, Dimba na Mtanzania akielezea jinsi walivyofanyakazi na Asha enzi za uhai wake.

Miongoni mwa waliohudhuria msiba huo ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wallace Karia na Katibu wake, Wilfred Kidao, Msemaji wa Simba SC, Haji Manara, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire wachezaji na wadau.

Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao akimzungumzia marehemu jinsi alivyoshirikiana na shirikisho hilo kufanikisha timu ya taifa na soka la hapa nchini kwa ujumla kufanya vizuri.

Akimuelezea marehemu enzi za uhai wake msibani hapo kwa niaba ya Kampuni ya Habari Cooparation, Mohammed Mharizo alisema yeye ni miongoni mwa wengi waliofundishwa kazi na marehemu ambaye hakuwa mchoyo wa kuwarithisha wengine kipaji chake.

Waombolezaji wakilia.

Waombolezaji wakiuswalia mwili wa marehemu.

Mwili ukipelekwa kaburini.

Wafanyakazi wenzake wakilia kwa huzuni.

Rais wa TFF, Wallace Karia (kulia) na Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire wakiwa kwenye msafara unaolekea makaburini.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/GPL
Toa comment

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *