ATCL Yarudisha Safari za Dar na Hahaya (Comoro)

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imerudisha safari za kawaida kati ya Dar es salaam (Tanzania) na Hahaya (Comoro) kuanzia 8/9/2020.

 

ATCL itafanya safari zake mara mbili kwa wiki, siku ya Jumanne na Jumapili. Abiria wote wanaotarajia kusafiri kwenda Comoro wanahitajika kuwa na cheti maalum kinachothibisha kuwa wamefanya vipimo vya COVID-19 na wajiandikishe katika ubalozi wa Comoro kabla hawajanunua tiketi.


ATCL wanawashukuru sana wateja wao kwa kundelea kuiamini Air Tanzania na kuendelea kutumia huduma zake popote pale tunaporuka.Toa comment