Atumia Nyoka kama barakoa kujikinga na Corona

12 0

Msafiri huyo aliyekuwa amevaa barakoa yake ya nyoka alikuwa amejizungushia katika shingo na mdomoni, alionekana katika basi lililokuwa linatokea Swinton kuelekea mji wa Manchester nchini Uingereza siku ya Jumatatu.

Mamla ya usafiri wa leri ya  Greater Manchester imesema kuwa nyoka hakubaliki kufunika uso kama barakoa

Abiria mmoja, alisema anadhani abiria huyo alikuwa amevaa barakoa ya kisasa tu mpaka alipomuona nyoka huyo akiteleza katika chuma cha kushikia mikono.

Mkuu wa usafirishaji wa Manchester amethibitisha kuwa alikuwa ni nyoka na sio barakoa halisi.

Shuhuda wa tukio hilo, ambaye alitaka kutofahamika alisema, ameona kuwa tukio hilo lilikuwa la kuchekesha na kustaajabisha,

Aliongeza kusema kuwa nyoka huyo hakuwasumbua abiria wenzake.

Msemaji wa usafiri wa Manchester alisema: “Muongozo uliotolewa na serikali umesema wazi kabisa kuwa barakoa zinazoruhusiwa sio lazima zile za upasuaji bali abiria anaweza kutengeneza barakoa yake anayoridhika nayo na kuivaa akiwa huru.

“Ingawa kuna kiwango kidogo tu tafsiri kamba inaweza kumaanisha hili, hatuamini maagizo hayo yalifikia kiwango cha mpaka kuruhusu ngozi ya nyoka-hususan wakati imeambatana na nyoka .”

Posted from

Related Post

DOGO SIMBA AMFUNGIA KAZI OKWI

Posted by - October 2, 2019 0
NA MAREGES NYAMAKA KASI ya zao la mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba, Miraji Athuman ‘Sheva’, imekuwa…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *