Aussems Akomaa na Wabrazili

WAKATI Ligi Kuu Bara ikiwa imesimama kupisha michezo iliyopo katika Kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameendelea kuwakomalia wachezaji wake Wabrazili kwa kuwafanyisha mazoezi katika Uwanja wa Gymkhana, Dar.

 

Kocha huyo ameendelea kuwapiga tizi nyota hao, Gerson Fraga na Tairone Santos ili wawe fiti zaidi baada ya kuanza kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania, Alhamisi iliyopita.

 

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu ameliambia Championi Jumatatu, kuwa kikosi hicho licha ya kutokuwa na mechi yoyote ya ligi lakini bado kimeendelea na programu yao ya mazoezi kama kawaida katika Uwanja wa Gymkhana.

 

“Sisi tunaendelea na mazoezi yetu na Jumamosi tumefanya katika Uwanja wa Gymkhana lakini pia  Jumapili tumefanya tena kwa mara nyingine.

 

“Mazoezi hayo yanahusisha wachezaji wote ambao wamebakia katika kikosi ukiwaondoa wale ambao wameenda timu zao za taifa kwa ajili ya mechi za kimataifa.

 

Lengo ni kuona wachezaji wanakuwa fiti zaidi wakati ambao tutarejea kwa ajili ya mechi zetu za ligi,” alisema Rweyemamu.

Said Ally na Lunyamadzo Mlyuka 

Toa comment