Azania Yadhibiti Corona Mbagala kwa Sabuni ya Champions

MAKAMPUNI ya Azania Group ambao ni mabingwa wa kutengeza sabuni zenye ubora wa hali juu za King Limau na Marhaba wakishirikiana na Global Group katika janga la Ugonjwa wa Covid 19 nchini, jana Ijumaa waliwaibukia wakazi wa maeneo ya Mbagala na kuwaosha mikono kwa sabuni ya Championi ambayo inasifika kwa kuua bakteria wa aina mbalimbali.

 

Kikosi hicho kikiwa na ndoo za maji na sabuni hizo kilipita maeneo ya Mbagala na kuanzia Ofisi ya Afisa Serikali ya Mtaa wa Kampochea Mbagala Rangi Tatu ambapo baada ya kupata baraka za viongozi wa ofisi hiyo walianza kuwanawisha wakazi wa maeneo hayo na kuwapa sabuni za bure.

 

Baada ya kutoka ofizi hiyo lilihamia Soko la Rangi Tatu na baadae Zakhiem, huku likiongozwa na Mwenyekiti wa Soko hilo, Hemed Njiwa akisaidiwa na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo, Habiba Mpunga.

 

Zoezi hilo lilionekana kuwafurahisha wafanyabiasha wakazi wengine waliokutwa maeneo hayo ambao waliisifu Kampuni ya Azania kwa kuja na sabuni hiyo kwa kipindi hiki cha janga la corona wengine wakiisifu sabuni hiyo kwa harufu yake nzuri.

 

“Unajua wengine hatuna vitakasa mikono majumbani au tunapotembea kwenye shughuli zetu sasa kipinde hiki cha sabuni ya Champions naweza kukihifadhi vizuri nikifika sehemu yenye maji nanawa mikono ili kujikinga na virusi vya corona”.

 

Alisema Dereva wa daladala Fikiri Magoso aliyepitiwa na kikosi hicho kwenye kituo cha mabasi cha Rangi Tatu Mbagala.

 

Sabuni hizo kwasasa zinapatikana kwenye maduka mbalimbali nchini kwa jumla na rejareja.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/GPL
Toa comment