Baada ya Kuzidiwa na Corona, Marekani Yaingakuia China

Baada ya kurushiana maneno kwa muda mrefu kila mmoa akimshutumu mwenzake kwamba ameleta janga la virusi vya corona, hatimaye Serikali ya Marekani na China wameamua kukaa meza moja na kuomba kushirikiana kwa pamoja ili kuudhibiti maambukizi na vifo vinavyotokana na ugonjwa Covid – 19.

 

Kupitia ukurasa wa Twitter wa Rais wa Marekani, Donald Trump, leo Machi 27, 2020, ameandika; “Nimemaliza kufanya mazungumzo mazuri na Rais wa China, Xi Jinping. Tumezungumza kwa kina kuhusu madhara makubwa yanayosababishwa na CoronaVirus katika sehemu kubwa ya dunia yetu. China amepitia hali hii kwa ugumu na amejenga uelewa mkubwa kuhusu virusi hivi. Tutafanya kazi kwa karibu na pamoja. Heshima kubwa kwao!”

Ikumbukwe kuwa, mpaka sasa Marekani ndiyo inaongoza kwa kuwa na watu wengi walioambukizwa CoronaVirus.

Marekani: wagonjwa 85,604
China: wagonjwa 81,340
Italy: wagonjwa 80,589.

 

 

 
Toa comment