Baba: Samatta Atafanya Makubwa Aston Villa

BABA mzazi wa mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta, mzee Ally Samatta, amesema anaamini mtoto wake atafanya makubwa msimu huu ndani ya Ligi Kuu England ‘Premier’.

 

Mzee Samatta ametoa kauli hiyo ikiwa bado siku chache kabla ya Premier kuanza Ligi Kuu England kuanza huku Aston Villa ikimuongeza mshambuliaji mwingine kutoka Birmigham City, Scott Hogan.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mzee Samatta alisema: “Kwanza niseme nafasi ya kijana wangu kucheza katika kikosi cha kwanza bado ipo tena kubwa sana licha ya huo usajili uliofanywa katika nafasi yake.

 

“Tofauti yake na wengine ni kwamba yeye amejaaliwa uwezo wa kucheza mipira ya chini na ya vichwa, naamini atafanya makubwa.

MJULIUS RICHARD NA CHRISTOPHER MABULA, DARToa comment