Balaa! Mapokezi ya Carlinhos Yatetemesha Yanga – Video

 

Rasmi kiungo fundi Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ (25) amewasili nchini tayari kuanza majukumu yake ndani ya mabingwa wa kihistoria, Yanga SC yenye maskani yake pale Mtaa wa Jangwani.

 

Carlinhos ametua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mchana wa leo Agosti 25, 2020 akipokelewa na Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said.

 

 

Mamia ya mashabiki wa Yanga wamejitokeza Uwanjani hapo kumpokea na kumlaki Carlinhos ambaye ni raia wa Angola.

 Toa comment