Balama Kuzikosa Mechi Nne Yanga

 

KIUNGO wa Yanga, Balama Mapinduzi, anatarajiwa kurejea uwanjani baada ya wiki nne kutokana na kutibu mguu wake wa kushoto ambao aliumia msimu uliopita wakati wa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC, hivyo atazitazama mechi nne mfululizo akiwa kwenye kochi.

 

Mechi hizo nne ambazo anatarajia kuzikosa ni hizi hapa:-6/09/2020, Yanga vs Tz Prisons, Uwanja wa Mkapa, 13/09/2020, Yanga Vs Mbeya City, Uwanja wa Mkapa, 19/09/2020 Kagera Sugar Vs Yanga, Uwanja wa Kaitaba na 27/09/2020 Mtibwa Sugar v Yanga, Uwanja wa Jamhuri.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha wa viungo wa Yanga, Riedon Berdien ambaye kwa sasa ndiye anayesimamia mazoezi ya timu hiyo, alisema kuwa Balama anaendelea vizuri hivyo atarejea uwanjani hivi karibuni.

 

“Balama anaendelea na programu yake kwa sasa kwani baada ya kupata majeraha msimu uliopita, alikuwa chini ya uangalizi wa jopo la wataalamu ambao wapo naye mpaka sasa.

 

“Kwa sasa anaendelea vizuri kwa mujibu wa ripoti na anaweza kuanza kuwa na wenzake baada ya wiki nne ama tatu, itategemea na ripoti kutoka kwa madaktari,” alisema Berdien.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

 Toa comment