Balinya aota kiatu cha dhahabu mapemaa

23 0


NA JESSCA NANGAWE

STRAIKA mpya wa Yanga, Juma Balinya, ameanza kuweka mipango yake sawa kuhakikisha anaifanyia mambo makubwa klabu yake hiyo. Balinya, raia wa Uganda, ni miongoni mwa wachezaji wapya waliotua ndani ya kikosi hicho msimu huu huku akiwa ni tegemeo kubwa kwa mashabiki kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao alioanza kuunoyesha.

Straika huyo tayari ameanza kuonesha mipango yake kwa kuivusha timu yake katika hatua ya pili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kufunga bao muhimu na la pekee dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Balinya alifunga bao hilo katika dakika ya 42 ya mchezo katika mechi iliyomalizika kwa kwa ushindi wa bao 1-0 na kuiwezesha timu hiyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 2-1 na sasa watakutana na Zesco katika mchezo ujao.

Balinya alisema, anafahamu ana kazi kubwa mbele yake lakini moja ya mipango yake ni kufanikiwa kufanya vyema kwenye michuano ya kimataifa pamoja na ligi kwa kufunga idadi kubwa ya mabao.

“Tuna kazi kubwa mbele yetu, kufanya vyema kwenye michuano ya kimataifa lakini pia kuhakikisha tunapigana kupata matokeo mazuri katika ligi ya nyumbani, lengo langu ni kuona nafunga idadi kubwa ya mabao hususan kwenye Ligi Kuu Bara ili nitimize ndoto yangu,” alisema Balinya.

Aidha amewataka wachezaji wenzake kushirikiana na kuwa kitu kimoja ili waweze kutimiza ndoto za klabu hiyo za kufika mbali kitaifa na kimataifa.Source link

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *