Balozi Kairuki: Watanzania Sitisheni Kuja China, Kuna Corona – Video

China imetangaza kuzuia wageni wote kuingia nchini humo hata kama wana viza au vibali, lengo likiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

 

China pia imeagiza ndege za nchi hiyo na zile za kigeni kufanya safari moja tu kwa wiki na hazitakiwi kujaza watu kwa zaidi ya asilimia 75.

 

Taarifa kutoka China zimeeleza kuwa kulikuwa na wagonjwa 55 nchini humo siku ya Alhamisi, kati yao 54 walikuwa ni wa kutoka nje ya nchi hiyo.

 

“Ikiwa ni mikakati ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona, kuanzia kesho Machi 28, 2020, Serikali ya China imesitisha VIZA zote za kuingia China na hati za ukazi (residence permit). Watanzania wenye VIZA na wanafunzi wenye hati za ukazi wasitishe mipango ya kurejea China hadi itakapotangazwa taarifa nyingine hapo tena.” amesema Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki.

 
Toa comment