Bao la Shakala laipa shavu Mbeya City

7 0


NA JEREMIA ERNEST

KAMPUNI ya Michezo ya Kubahatisha ya Parimatch Tanzania, leo imeingia rasmi mkataba wa kuidhamini Mbeya City inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao (2020-21).

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana, amesema mkataba huo ni faida kwa klabu hiyo si tu katika ligi, bali kwenye michuano mingine itakayoshiriki.

“Tunaamini kuwa mwanzo huu utafungua milango ya ushirikiano na klabu na ligi zingine ambazo Parimatch inadhamini kimataifa,” amesema Maligana.Ameongeza kuwa walipanga kuanza na klabu yenye ushawishi, hivyo wakaona Mbeya City ina kigezo hicho.

“Mbeya City ni Klabu kubwa kwa hapa Tanzania, hususan ukiangalia idadi ya mashabiki. Parimatch ni kampuni inayohudumia na kujali watu wote ingawa tumeanza na Mbeya City,” amesema.

Wakati huo huo, Maligana amemtaja mshindi wa tuzo ya bao bora kwa msimu uliopita wa Ligi Kuu, Paston Shikala, akisema amewavutia pia kupeleka udhamini wao Mbeya City.


“Baada ya kuona lile goli la Paston Shikala ambalo ndilo bora kwa msimu (uliopita), nasi tukaona huku ni kuzuri. Tutaenda kwa vilabu vingine pia, iwe Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza, ikiwa ni kuunga mkono juhudi za TFF na Bodi ya Ligi katika kuhakikisha ligi za Tanzania zinakuwa na tunaenda kimataifa,” anasema.Source link

Related Post

Sitaki Tena Mazungumzo na China

Posted by - May 15, 2020 0
Trump: Sitaki Tena Mazungumzo na China May 15, 2020 by Global Publishers UHUSIANO kati ya Marekani na China umeendelea kuzorota…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *