Benki ya NMB yafungua tawi Malinyi mkoani Morogoro

3 0

Benki ya NMB imeendelea kupanua wigo wake kwa kufungua tawi ‘NMB Malinyi’ katika wilaya ya
Malinyi Mkoani Morogoro. Ufunguzi wa tawi hili umeleta ahuweni kwa wakazi waliokuwa wanasafiri.


umbali wa kilomita 160 kwenda mji wa Ifakara Wilayani Kilombero kupata huduma za kibenki.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Malinyi – Mathayo Masele
amesema tawi hilo limekuwa likisubiriwa kwa hamu sana kwani NMB ndio taasisi ya kwanza kufungua
tawi ambapo anaamini litachochea ukuaji   wa uchumi na maendeleo katika eneo hilo kutokana na
kuongezeka kwa kasi ya uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo pamoja na uchimbaji wa madini ya
dhahabu ambayo yamegunduliwa hivi karibuni.
Masele alisema kuwa Benki hiyo licha ya  kukuza uchumi pia itawapunguzia gharama wafanyabishara, na
Taasisi ambazo zilikuwa zikitumia gharama kubwa kwaajili ya kusafirisha fedha kwa usalama zaidi
Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Salie Mlay, alisema moja ya
kichocheo kikubwa cha kufungua tawi hilo ni kuwasaidia wakulima na wafugaji waweze kupata mikopo.


pamoja na elimu ya ushirika utakaowapa tija kwa kutumia mfuko wa NMB Foundation.
Sambamba na uzinduzi huo, NMB imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi vikiwemoa mabati, kofia,
misumari na mbao kwaajili yakukamilisha uwezekaji vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi
Nawigo iliyopo Malinyi. Ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.

Posted from

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *