Bernard Membe “Nimeitwa kwenye kikao cha kamati ndogo ya Udhibiti na Nidhamu Dodoma nitahudhuria mapema bila kukosa”

29 0

Waziri wa zamani wa mambo ya nje Bernard Membe amethibitisha kuitwa kwenye kikao cha kamati ndogo ya Udhibiti na Nidhamu huku akithibitisha kuhudhuria ingawa hajaweka wazi ameitwa kwenye kamati hiyo ya chama cha Mapinduzi CCM au ni kamati ipi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Membe ameweka ujumbe huo huku akithibitisha kuhudhuria mapema bila kukosa, Pia Membe ameweka wazi kuwa Kikao hicho kinatarajia kufanyika Februari 6, 2020.

Ujumbe huo unasomeka hivi:-

“Hatimaye, jana jioni nimepokea barua ya kuitwa kwenye kikao cha Kamati ndogo ya Udhibiti na Nidhamu Jijini Dodoma. Kikao kitafanyika tarehe 6/02/2020 saa 3 Asubuhi kwenye jengo la White House. Nitahudhuria bila kukosa na bila kuchelewa! Stay tuned!”

Posted from

Related Post

Lulu Atoa Kali Ya Mobeto

Posted by - February 15, 2020 0
Lulu Atoa Kali Ya Mobeto February 15, 2020 by Global Publishers Staa machachari wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *