Bilionea wa Nigeria awanunulia mabinti zake watatu Ferrari, Davido aahidi kumnunulia binti yake (+Video)

4 0

Bilionea wa Nigeria, Femi Otedola ameibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuwanunulia mabinti zake watatu gari aina ya Ferrari Portofino kila mmoja.

Watoto hao wakike wa Bilionea, Otedola ni Tolani Otedola, Temi Otedola na Florence Otedola (DJ Cuppy).

Kupitia akaunti yake ya Twitter, DJ Cuppy amefunguka kuwa Mr Otedola amewanunulia kila mmoja gari aina ya  Ferrari Portofino, inakadiriwa kuwa dola 218,750 za Marekani. Gari hilo sio kubwa sana ila lina injini yenye muundo wa V8 lakini mwendo wake ni wa kasi mno.

“Baba yetu alitupeleka dukani na kutununulia kila mtu gari lake!”, kwa mujibu wa ujumbe uliowekwa kwenye Twitter na Temi Otedola.

Kwa mujibu wa Wikipedia inaonesha Femi Otedola ana utajiri wa thamani ya zaidi ya dola bilion 1.85 pesa za Marekani.

Davido ahamasika na walichofanyiwa mabinti wa tajiri wa Nigeria Femi Otedola, na alimjibu moja kati ya mabinti wa Mzee huyo, Florence Otedeola maarufu kama DJ Cuppy 

 

Davido aliandika kuwa ” Congrats Cupp …..! I will do the same for my daughters one day amen… chai money good.

 

Mwezi Julai 2019, tajiri huyo aliwapeleka mabinti zake mapumzikoni mjini Monaco nchini Ufaransa. Wakiwa mapumzikoni nchini humo, alitumia Saa 1 kuwapeleka nchini Italia kununua Ice cream na kisha kurejea tena Ufaransa.

Posted from

Related Post

Mjengo wamuumbua Mke wa Rayvanny

Posted by - February 20, 2020 0
Mjengo wamuumbua Mke wa Rayvanny February 20, 2020 by Global Publishers AMEUMBUKA! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na mjengo ambao mke…

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *