Bonge la Nyau Aanika Alichokiona Kabla ya Ajali

MSANII nchini ajulikanaye kama Bonge la Nyau amesema kitu cha mwisho walichokiona kabla ya kutokea kwa ajali ambayo aliipata na wenzake hivi karibuni, ni mwanga mkali mbele yao, kisha Lulu Diva akaanza kupiga kelele za “Mama Nakufaaa!”

 

Amesema baada ya hapo waliona lori kubwa mbele yao ndipo dereva wao alipoamua kulitupa gari kwenye makorongo ili mradi wasigongane uso kwa uso maana ndiyo ingekuwa mbaya zaidi kwa upande wao.

 

“Lori na lori yalikuwa yanashindana kwenye ku-overtake kisha lori moja likaingia kwenye njia yetu, ghafla tukaona mwanga mkali sana kwenye gari letu, mara nikaanza kusikia kelele za Lulu Diva akisema ‘mama nakufa, mama nakufa’.

 

“Dereva wetu alikuwa kwenye mwendo mkali na ilikuwa usiku hivyo akalitupa gari kwenye korongo ili mradi tusigongane uso kwa uso maana ndiyo ingekuwa mbaya zaidi,” ameeleza.

 

Msanii huyo, Lulu Diva na Belle 9 walipata ajali ya hiyo maeneo ya Chalinze wakati wakirejea jijini Dar es Salaam baada ya kutoka kwenye kampeni za Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Kilolo, Iringa.Toa comment