Bongo 255 Yahamia Mtaani, Balaa la Chid Benz Ilala Hatari Tupu – Video


SHOO namba moja ya burudani nchini, Bongo 255 inayoruka kupitia +255 Global Radio, leo Ijumaa, Septemba 25, 2020 imetoka studio na kuhamia mtaani katika viunga vya Soko la Ilala ili kujitambulisha kwa wasikilizaji na wafuatiliaji wa kipindi hicho ambao wengi wao wapo mtaani.

 

Mashabiki wa shoo hiyo wameweza kukutanishwa na wasanii mbalimbali LIVE akiwemo msanii nguli wa Bongo Fleva, rapa Rashid Makwiro aka ‘Chid Benz’, Morta the Future na Saigon ambao wamefanya makamuzi ya kibabe mbele ya mashabiki wao.

 

Mbali na kufanya makamuzi, mashabiki wamepata fursa ya kupiga stori na mastaa hao LIVE na kuwauliza maswali kadhaa wa kadhaa huku wasanii hao pia wakijibu jambo ambalo linawafanya kuendelea kuwa karibu na mashabiki wao.

 

Bongo 255 huruka kila Jumatatu mpaka Ijumaa kupitia +255 Global Radio kuanzia saa 6:00 mchana mpaka saa 10:00 jioni.

TAZAMA SHOPO NZIMA HAPA
Toa comment