Bosi Man U Afunguka Mpango wa Kumtimua Solskjaer

SAA chache kabla ya kuivaa Liverpool katika Premier League, bosi wa Manchester United, Ed Woodward amejitokeza na kumuunga mkono kocha wake, Ole Gunnar Solskjaer akimuunga mkono na kudai kuwa
hakuna mpango wa kumfukuza.

 

Ikiwa United itapoteza mchezo huo wa kesho Jumapili, kibarua cha Solskjaer kitakuwa hatarini na imekuwa ikitajwa kuwa yupo njiani kufukuzwa lakini Woodward ambaye ni mtendaji mkuu wa klabu hiyo amesema anamuunga mkono kocha kwa asilimia 100.

 

“Tunatakiwa kushinda mataji, tunatakiwa kucheza soka la kushambulia na tunatakiwa kuwapa chipukizi nafasi.

 

Alipofika katikati ya msimu uliopita alionyesha anaweza kuyafanya hayo kwa vitendo. “Timu ilianza kucheza kwa kasi, kwa staili na katika falsafa ya kocha ambayo alikuwa akiitaka,” alisema bosi huyo na kuongeza: “Ole amerejesha nidhamu kwenye klabu, wachezaji wanaheshimiana na hakuna mkubwa kuliko klabu.”

 

Aidha, Woodward amesisitiza kuwa suala la mataji ndilo la muhimu kabla ya wao kuangalia faida ambayo inapatikana kwenye fedha, akiamini mataji yakija na fedha zitafuata.

 

 

United haijashinda taji la Premier League tangu Sir Alex Ferguson alipostaafu mwaka 2013 lakini kwa sasa timu hiyo inashika nafasi ya 12 katika Premier ikiwa ni takwimu mbaya kuwahi kutokea klabuni hapo kwa miaka 30.

Toa comment