Breaking News: Kim Jong-Un Aonekana Hadharani

KWA mujibu wa Vyombo vya Habari nchini Korea Kusini, Kim Jong-un ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza baada ya siku 20 akiwa anakata utepe kwenye uzinduzi wa kiwanda cha mbolea.

 

Shirika la habari la Taifa, KCNA limeeleza kuwa Kim aliambatana na Maafisa kadhaa wa Korea Kaskazini akiwemo dada yake Kim Yo Jong, jambo lililofanya watu waliokuwepo kiwandani hapo kushangilia kwa furaha.

 

Haya hivyo, Shirika hilo la habari halikutoa picha zozote wala kuelezea wapi alikuwa Kiongozi huyo. Naye Rais wa Marekani, Donald Trump alipouliza amejibu “Siwezi kusema chochote kwa sasa.”

 

 

Taarifa kuhusu hali mbaya ya afya ya Kim ilianza kusambaa baada ya Kiongozi huyo kukosa kushiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Babu yake ambaye ni Mwanzilishi wa Taifa hilo, Kim II Sung mnamo Aprili 15, 2020.

 

Maadhimisho ya kumbukumbu hiyo ni tukio kubwa sana katika matukio ya nchi hiyo, na Kim mara zote hutembelea alipozikwa babu yake na hajawahi kukosa tukio hilo hapo kabla.

 

Shirika la Habari la Korea Kaskazini, KCNA limeachia picha kadhaa kumuonesha Kiongozi wao Kim Jong-un akikata utepe katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kiwanda cha mbolea.

 
Toa comment